
KLABU ya Simba imetangaza kukamilisha usajili wa Kiungo Victor Patrick Akpan kutoka Coastal Union raia wa Nigeria kwa mkataba wa miaka miwili.
Akpan amesajiliwa ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo huku akitajwa kama mbadala sahihi wa Mganda Tadeo Lwanga ambaye huenda akatolewa kwa mkopo.
Mnigeria huyo alikuwa nguzo muhimu kwa Coastal kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam Azam Sports Federation Cup na kufanikiwa kuifiksha fainali ambayo walipoteza mbele ya mabingwa wa ligi kuu, Yanga kwa mikwaju ya Penati.