
RAIS wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa (73) ametoroka nchi yake kwa kutumia ndege ya jeshi la nchi hiyo akiwa yeye mke wake pamoja na maafisa wawili wa Serikali.
Taarifa zinadai amekimbilia katika kisiwa cha Maldive kilichopo kusini Magharibi mwa nchi ya Sri Lanka hiyo ni kufuatia maandamano ya kupinga utawala wake ambayo yanaendelea nchini humo.
Kabla ya kutoroka nchi yake Rais Gotabaya amemteua Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe kuwa Kaimu Rais wa nchi hiyo.

Kutimka kwa Rais huyo kunatajwa kumaliza utawala wa familia hiyo ambao umedumu kwa zaidi ya karne mbili katika siasa za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichoiambia BBC kimethibitisha kuwa Rais huyo hatarajii kuendelea kuishi katika visiwa hivyo vya Maldive na badala yake ataondoka na kukimbilia kwenye nchi nyingine ya tatu.
Aidha nduguyake Basil Rajapaksa ambaye alikuwa Waziri wa Fedha naye ameripotiwa kutimka nchini humo na anadaiwa kukimbilia nchini Marekani.