×

Manara Athibitisha Yanga Kuweka Kambi Avic Town, Atangaza hatma ya Ushindi

Msemaji wa Yanga Haji Manara

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga Haji Manara amebainisha kuwa klabu yake itaweka kambi katika eneo la Avic Town lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/2023.

 

Akiongea na waandishi wa habari Manara amesema miundombinu imeimarishwa katika kambi ya Avic Town na nyota mbalimbali wa klabu hiyo wataanza kuripoti kambini kuanzia kesho Julai 20, 2022.

 

Aidha Manara amebainisha kuwa Benchi la Ufundi la Klabu hiyo limepanga kuja na Programu maalum kwa ajili ya wachezaji hasa ikiwemo kuhusu mazoezi ya viungo.

Chico Ushindi wa Kubanza ameachwa na Klabu ya Yanga

Kulikuwa na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zikibainishakuwa Yanga ilipanga kwenda kufanya maandalizi yake ya msimu mpya nchini Uturuki taarifa ambazo hazijathibitishwa na klabu ya Yanga.

 

Aidha Manara amethibitisha klabu yake kuachana na mchezaji Chico Ushindi wa Kubanza ambaye mkataba wake wa kuhudumu ndani ya klabu hiyo kwa mkopo kutokea TP Mazembe umemalizika na Yanga kama Klabu imeamua kumruhusu mchezaji huyokurudi katika klabua yake ya TP Mazembe.

Leave a Comment