
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri MKuu Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako ametoa maelekezo ya kupata orodha ya mashirika,Taasisi, Halmashauri na Majiji ambayo hayawasilishi michango ya wanachama wa mifuko mbalimbali ya jamii
Aidha ametumia nafasi hiyo kutoa maelekezo kwa mifuko ya pensheni kutatua changamoto ambazo zinasababisha wastaafu kuchelewa kupata pensheni zao au kupunjwa fedha zao hali inayosababisha kuendelea kwa malalamiko ambayo yangeweza kupata ufumbuzi wa haraka