×

Man X: Sisikilizi Nyimbo za Diamond, Haziniingii Kabisa Kichwani na Siwezi Kuziimba

Man X

MSANII mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Man X amefanya mahojiano na 225 Global Radio kwenye kipindi cha Bongo 255 ambapo amesema kuwa pamoja na kuwa nje ya game kwa muda mrefu na kutambua mabadiliko ya muziki lakini bado haukubali mziki anaoimba Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kwa sababu ngoma zake hazimuingii kichwani.

 

Man X amesema mara nyingi anapenda kusikiliza ngoma kutoka Uingereza kwasababu kuna vitu anataka kujifunza kuhusu ngoma za wasanii wa ndani amebainisha kuwa hawa wapo tu.

Man X amefanya mahojiano na 255 Global Radio na Global TV

Alipoulizwa kuhusu wasanii anaowakubali hapa nchini amewataja Profesa Jay, Sugu, Afande Sele, AY pamoja na Dully Sykes.

 

Aidha, amewataja wasanii ambao wanatakiwa kuheshimiwa kila siku kutokana na mchango wao kwenye tasnia ya muziki nchini ambapo amewataja Profesa Jay, Sugu, P- Funk, Master Jay pamoja na Bizman.

Man X amesema amerudi rasmi kwenye game ya muziki wa Bongo Fleva

Sambamba na hayo Man X ametangaza kuachia ngoma yake mpya ya Nyepenyepe huku akisisitiza kuwa amerudi rasmi na anaomba mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva wampokee katika ujio wake mpya.

Leave a Comment