The House of Favourite Newspapers

Rihanna Aachia Kipande Kingine cha AntiDiary: Room 7

0

rihanna-crownANTIDIARY ROOM 7
ANTIDIARY ROOM 6

 DIVA wa muziki wa Pop, Rihanna kwa kushirikiana na Kampuni ya Sumsung, ameendeleza kuwatega mashabiki wake ikiwa ni mwanzoni tu mwa mwaka huu mpya wa 2016 baada ya kuachia kipande kingine cha video alivyoviita ANTIdiaRY ambapo ameachia chumba namba saba (ANTIdiaRy: Room 7).

Katika chumba hicho cha saba, Rihanna anaoenekana akiingia ofisini akiwa amevalia nguo nyeusi. Anasalimiwa na bibi kizee aliyeketi kwenye kiti, bibi huyo anamuonesha Rihanna milango miwili ya dhahabu ambapo anatakiwa aelekee.

Baaada ya kufungua milango hiyo na kuingia ndani anakuta wahasibu kwenye chumba kilichotengenezwa kwa dhahabu wakiwa ‘bize’ kuandika kwenye vifaa vya kiteknolojia vilivyotengenezwa kwa dhahabu pia.

Baadaye anatokea binti aliyevalia taji la dhahabu kichwani mwake, taji ambalo linaonekana kuwepo kwenye kava ya albamu yake mpya ya ANTI. Binti anavua taji na kumpa Rihanna ambapo naye analipokea na kulivaa kisha chumba cha saba kinakuwa giza ghafla.

Rihanna aliamua kufanya hivyo kwa lengo la kuwavuta karibu mashabiki wake wenye shauku ya kuipata aolbamu yake mpya na ya nane ijulikanayo kama ANTI.

Rihanna anatarajia kuanza kufanya ‘tour’ ya ANTI World kwenye miji ya San Diego, Calif huko Amerika Kaskazini.

Leave A Reply