The House of Favourite Newspapers

Shule ya Msingi Hazina Yaongoza Mock Darasa la Saba Kinondoni

0
Mkuu wa shule ya Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam Omar Juma akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Iptusm Ramadhani kwa kuwa wa kwanza kwenye mtihani wa utamilifu shuleni hapo
·    

SHULE ya Msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam, imeongoza kwenye matokeo ya mtihani wa utimilifu (Mock), darasa la saba kwa Wilaya ya Kinondoni.

Kwenye matokeo hayo yaliyotolewa na Mkoa wa Dar es Salaam, hivi karibuni, shule hiyo imeshika nafasi ya kwanza kati ya shule 158 za wilaya hiyo.

 

Mkuu wa shule hiyo, Omar Juma, alisema jana kuwa shule hiyo iliongoza kwenye mtihani uliofanyika mwezi wa nne na ule uliofanyika mwezi wa saba mwaka huu.

Mkuu wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni Dar es Salaam, Omar Juma, akimpa zawadi mwanafunzi wa darasa la saba Cassie Mazwile, aliyeshika nafasi ya tatu shuleni hapo

 

Alisema  walimu wake wamekuwa wakijituma kuwaandaa wanafunzi hao kwaajili ya mitihani ya ndani na ile ya kitaifa na kwamba hiyo ndiyo imekuwa siri kubwa ya mafanikio kwao.

 

Alisema kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa wanafunzi hao wanaimani kwamba watafanya vizuri zaidi pia kwenye mtihani wa kitaifa wa darasa la saba mwaka huu.

 

“Sisi tunapiga kazi hapa ni kazi tu nawashukuru walimu kwa kuifanya shule hii kuongoza mtihani wa utamilifu kwa mara ya pili mfululizo hii inatupa moyo wa kuendelea kufanyakazi,” alisema Omar

Wanafunzi wa shule ya msingi Hazina ya Magomeni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja na tuzo mbalimbali

 

Alisema kujituma kwa walimu na ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata kwa uongozi wa shule na wanafunzi ndiyo kitu wanachojivunia.

 

“Walimu wanafanyakazi kwa moyo sana, wazazi wa wanafunzi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri sana kwa shule na uongozi wa shule unawajali sana walimu, hayo kwa pamoja yamekuwa yakisaidia ufaulu wetu kuwa juu mwaka hadi mwaka,” alisema

 

Aliwapongeza wanafunzi kwa mafanikio hayo na kuwataka wasome kwa bidii ili hatimaye waweze kuendelea kuongoza kitaifa na  Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mitihani ijayo.

Leave A Reply