×

Dullah Mbabe Kuzichapa Leo, Dully Sykes, Mr Blue Kunogesha Pambano

Dullah Mbabe

 

BONDIA mwenye tambo nyingi mchezoni Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe, leo anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na bondia, Kahoro Kahumwa kwenye pambano lisilo la ubingwa ambalo litachezwa kwenye Ukumbi wa The Kukuz uliopo Makonde Mbezi Juu jijini Dar.

Kahoro Kahumwa

 

Akizungumza na mwandishi wetu mratibu wa pambano hilo, Makuku Silvester Mgaya amesema pambano la wababe hao litatanguliwa na mapambano wengine ya utangulizi wakiwemo wababe wa kike wenye upinzani mkali, Feriche na Zainab.

Mkurugenzi wa The Kukuz Pub, Makuku Sylivester Mgaya mratibu wa pambano hilo.

 

Makuku amesema pamoja na pambano hilo mashabiki watapata burudani kutoka kwa wakali wa Bongo Fleva, Dully Sykes na Mr Blue ambao watapiga shoo kali kunogesha pambano hilo.

Prince Dully Sykes naye atatoa burudani ya muziki kwenye ndonga hizo.

 

Mratibu amesema pamoja na burudani zote hizo watakaofika ndani ya The Kukuz kwa ajili ya pambano hilo pia watainjoi matukio mbalimbali ikiwemo kinachoendelea kwenye tamasha la Simba Day kupitia runinga kubwa zilizowekwa kona mbalimbali mbalimbali.

Leave a Comment