×

Barca Yakamilisha Usajili wa Nyota Wake Wapya, Kounde Matatani

Robert Lewandowski

KLABU ya Barcelona ya nchini Hispania imekamilisha kuwaandikisha wachezaji wake wanne kati ya watano waliosajiliwa na klabu hiyo kuelekea katika mashindano mapya ya msimu huu wa 2022/2023.

 

Barcelona imetengeneza kiasi cha Euro milioni 85 baada ya kuuza haki zake za matangazo ya studio kwa kampuni ya Orpehus Media lakini mchezaji mpya Jules Kounde ameshindwa kuandikishwa kuelekea mchezo wa kwanza wa klabu hiyo dhidi ya Rayo Vallecano mwisho wa wiki hii.

Raphinha

Wachezaji ambao tayari wamesha andikishwa ni pamoja na Robert Lewandowski, Raphinha, Franck Kessie pamoja na Andres Christensen.

 

Ousmane Dembele pamoja na Sergi Roberto nao tayari wamefanikiwa kuandikishwa baada ya kuongeza mikataba mipya ya kuendelea kuhudumu ndani ya Camp Nou.

Franck Kessie

Aidha Barcelona inatarajia kukamilisha dili la kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Marcos Alonso pamoja na Bernardo Silva wa Manchester City ambaye anatajwa kuwa ndiyo kipaumbele katika usajili wa msimu huu.

 

 

 

Leave a Comment