
ALIYEKUWA mgombea wa Chama cha UDA kwenye uchaguzi wa Rais nchini Kenya William Ruto amechaguliwa kuwa Rais mteule wa awamu ya Tano wa Serikali ya Jamhuri ya Kenya.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) Wafula Chekubaki amebainisha kuwa licha ya kuwa na changamoto kadhaa ikiwemo vitisho pamoja na kushikiliwa kwa baadhi ya viongozi wa Tume hiyo lakini ameswashukuru wakenya kwa kumaliza uchaguzi salama.

Naye mgombea kupitia Chama cha Azimio Raila Odinga ameshindwa kutokea katika hafla ya kutangazwa kwa Rais Mteule huyo.

Kwa mujibu wa Wafula Chekubaki William Ruto amepata jumla ya kura 70,176,141 ambayo ni sawa na 50.49% huku mpinzani wake Raila Odinga akipata jumla ya kura 60,942,930 ambayo ni sawa na 48.85%.