×

Wesley Fofana Alilia Kuachana na Leicester City, Ni Baada ya Kuhitajika na Vigogo wa London

Wesley Fofana

KLABU ya Leicester City kwa muda mrefu iliweka msimamo juu ya mchezaji wao beki kitasa wa kati Wesley Fofana kuwa hauzwi, lakini kwa siku za karibuni mchezaji huyo ameonekana kuvutiwa na ofa mbalimbali kutoka katika klabu kubwa katika ligi hiyo ya Uingereza.

 

Fofana ambaye hivi karibuni aliongeza mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo yenye makazi yake jijini Leicester mpaka mwaka 2027 ameonekana kuvutiwa na ofa kutoka katika klabu ya Chelsea ya London huko Uingereza.

Thomas Tuchel

Klabu ya Chelsea hadi sasa imetuma ofa mbili kwa dau la Euro milioni 60 na milioni 65 lakini zote zimekataliwa na Mbwa mwitu hao wa jiji la Leicester wakidai kuwa gharama halisi ya kuvunja mkata wa mchezaji huyo ni Euro milioni 80.

 

Leicester City wanaonekana kutokuwa tayari kumuachia mchezaji huyo lakini kwa upande mwingine wanaonekana hawatakuwa na namna ya kumzuia iwapo Chelsea watafikia dau hilo la Euro milioni 80.

Wesley Fofana anataka kuondoka Leicester City na kujiunga na klabu ya Chelsea

Chelsea wanamuhitaji beki huyo ili kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya kukamilisha usajili wa Kalidou Koulibaly na Marc Cucurella, ambapo kocha wa Chelsea Thomas Tuchel atakuwa na nafasi nzuri ya kutumia mfumo wa mabeki watatu nyuma ambapo atawatumia Koulibaly , Thiago Silva na Fofana huku Reece James na Cucurella wakitumika kama ‘wing-backs’.

 

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment