×

UN na Ukraine Wakubali Kuyamaliza na Urusi, Ni Baada ya Vita Kusogelea Sehemu Hatari

 

Katibu mkuu umoja wa mataifa UN

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres pamoja na marais wa Uturuki na Ukraine wamejadili namna za kumaliza vita vilivyoanzishwa na Urusi nchini Ukraine ili kulinda kinu kikubwa Zaidi cha nishati ya nyuklia barani Ulaya.

 

Guterres amewaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo mjini Lviv kwamba ana wasiwasi sana kuhusiana na yanayoendelea katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia. Guterres ametaka wanajeshi na silaha kuondolewa nchini humo.

 

“Ni lazima akili itumike ili kusiwepo na vitendo vitakavyohatarisha usalama wa kiwanda hicho cha nyuklia. Kinu hicho hakistahili kutumika kama sehemu ya operesheni yoyote ya kijeshi badala yake, kunahitajika makubaliano ya dharura ili kuhakikisha kwamba Zaporizhzhia ni muundo msingi wa kiraia na kuhakikisha usalama wake.” Alisema Guterres alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Wataka kumaliza vita dhidi ya Urusi

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan, Guterres na Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky wanaangalia njia nzuri Ya amani ambayo itaenda kumaliza vita hii na kuacha sehemu kubwa ya ulaya kuwa na amani.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa Global Tv

Leave a Comment