
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Zainab Kawawa akishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Kilwa, Ali Kasinga wamefanya bonanza la jogging pamoja na wakazi wa maeneo hayo wakihamsisha sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu pamoja na kuchangia damu.

Bonanza hilo ambalo lilianza mapema asubuhi ambapo washiriki hao walizunguuka pande mbalimbali za wilaya hiyo huku wakihamasisha wananchi kuhakikisha wanahesabiwa ifikapo Agosti 23 mwaka huu.

Baada ya jogging kilichofuatia ni uchangiaji wa damu ambapo DC Zainab na Mbunge Kisinga ndiyo waliongoza zoezi hilo kwa kujitolea damu.