
RAIS Volodymyr Zelensky wa Ukraine anahofia kwamba huenda Urusi ikafanya mashambulio makubwa wakati nchi yake inapotarajia kuadhimisha miaka 31 ya uhuru wiki ijayo.
Mamlaka katika mji mkuu, Kyiv, zimetangaza kukataza mikusanyiko ya watu, na katika mji wa Kharkiv imeweka marufuku ya kutotoka nje siku yenyewe ya uhuru.
Ukraine inatarajia kusheherekea siku yake ya uhuru tarehe 24 agosti siku ambayo pia itakuwa ni kumbukumbu ya miezi sita tangu Urusi kuivamia nchi hiyo.

Mshauri wa rais, Mykhaylo Podolyak, alisema kwamba Urusi inaweza kuongeza mashambulizi yake ya kijeshi siku hiyo.
“Urusi ni dola la kale ambalo linafungamanisha matendo yake na tarehe maalum, ni aina fulani ya imani ya ndani,” shirika la habari la Interfax-Ukraine lilimnukuu akisema.
“Wanatuchukia na watajaribu kuongeza idadi ya mashambulizi ya mabomu kwenye miji yetu ukiwemo Kyiv wakitumia makombora kutokea baharini,” alisema Podolyak.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao