
SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mifigo na Uvuvi imetenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vikundi maalumu vya wavuvi wa Samaki jijini Mwanza nchini Tanzania.
Hatua hii imekuja katika kipindi hiki ambacho serikali ipo kwenye mikakati ya kukuza na kuboresha uchumi wa bluu nchini Tanzania, huku ziwa Viktoria lililopo jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya sehemu zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi huo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega akiongea alipotembelea Wilaya za Ilemela na Ukerewe jijini Mwanza alisema “Vijana wengi waingie kwenye kazi hii(Uvuvi), mheshimiwa Mkuu wa Wilaya wapange hao vijana, pesa zipo tutawaletea”.
Pia Naibu Waziri Ulega akaeleza adhima ya serikali katika kuinua sekta ya uvuvi kama njia ya kutatua changamoto ya ajira kupitia ufugaji wa Samaki kwa njia ya Vizimba, Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kwaajili ya kuwasaidia wavuvi na wafugaji wa Samaki katika ziwa Viktoria jijini Mwanza.
Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.