×

Ukweli wa Mtangazaji Diva TheBawse Kushindwa Kupata Mtoto – Video

Diva na Mumewe Abdulrazack kwenye kipindi cha mapito

MTANGAZAJI wa kipindi cha Lavidavi kinachoendeshwa kupitia wasafi media ametoa ya moyoni wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Mapito kinachofanywa na Studio za 255Globalradio na Global TV.

 

Katika kipindi hicho cha Mapito Mtangazaji Alimuuliza swali Mume wa Diva ambaye aliongozana naye katika kipindi hicho, Abdulrazack kuhusu kuwa na mtoto na historia yake ya kushindwa kupata mtoto katika nyakati tofauti.

 

“Nilichogundua mimi kwa miezi saba niliyokua naye ni kwamba Diva hana shida ya uzazi na mpaka sasa ameshashika mimba mara tatu isipokua mfuko wake wa uzazi upo dhaifu” alisema mume wake Abdulrazack.

Abdulrazack mume wa mtangazaji Diva the bawse

Aliendelea kwa kusema kuwa ili aweze kupata mimba ambayo itamfanya apate mtoto itabidi apate muda wa kupumzika kwa miezi mitatu ambapo kitu hicho ni kigumu kutokana na kazi anazozifanya alimalizia Abdulrazak amabaye ni Mume wa ndoa wa Diva.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa Global Tv

Leave a Comment