MARUBANI katika shirika la ndege la Ujerumani la Lufthansa watafanya mgomo wa siku nzima hapo kesho Ijumaa. Mgomo huo utaathiri ndege zote za abiria na mizigo za shirika hilo kutoka Ujerumani.

Tangazo hilo limetolewa kufuatia mazungumzo ya kina na kampuni pamoja na ombi la kamati ya pamoja ya majadiliano.
Mazungumzo juu ya makubaliano mapya ya mishahara yameshindwa kuzaa matunda, licha ya duru kadhaa za majadiliano.

Chama cha wafanyakazi Marubani kinataka nyongeza ya aasilimia 5.5 ya mshahara kwa mwaka huu na nyongeza ya moja kwa moja kwa ajili ya mfumuko wa bei kuanzia mwakani.
Pia kumekuwa na mivutano ya chini kwa chini kuhusu mkakati wa siku za usoni wa kampuni ya Lufthansa.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mtandao