
RAILA Odinga mgombea wa kiti cha uraisi wa Azimio la Umoja alipoteza tena kwa mara ya tano dhidi ya mpinzani wake Willium Ruto aliyetangazwa mshindi kwa asilimia 50.49% huku Raila akivuna asilimia 48.85%.
1997-kupitia chama chake cha National Democratic Party alichokiunda baada ya kujiondoa chama cha Forum for the Restauration of Democracy-Kenya (FORD-K) Raila Odinga aligombea nafasi ya kiti cha Urais na kushindwa.
2002-kupitia chama cha Liberal Democratic Party (LDP) waliungana na National Alliance of Kenya (NAK) na kuunda National Rainbow Coalition (NARC) iliyomshinda Uhuru Kenyatta lakini mwaka huu Raila Odinga hakuwania kiti cha uraisi.
2007-Raila Odinga aliingia tena kwenye mbio za kuwania kiti cha urais kwa mara ya pili dhidi ya Mwai Kibaki na kushindwa.
2008-Raila aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Kenya na hii ilikuja baada ya machafuko yaliyosababishwa na wafuasi wake kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo yalisababisha vifo vya raia wa Kenya zaidi ya elfu mbili.

2013- Raila aliingia kwa mara nyingine kwenye kinyang’anyiro cha kiti cha urais na hii inakuwa ni mara ya tatu kupitia chama chaCoalition for Reforms and Democracy (CORD) dhidi ya mpinzani wake Uhuru Kenyatta na kushindwa.
2017- Raila aligombea tena nafasi ya Uraisi kwa mara ya nne kupitia chama cha NASA dhidi ya mpinzani wake Uhuru Kenyatta na alishindwa.Odinga alipinga matokeo ya uchaguzi huo mahakamani kuwa ni batili na kutaka uchaguzi urudiwe, na baadaye akatangaza kujiondoa rasmi kwenye uchaguzi.
2022-aliwania kiti cha urais kwa mara ya tano kupitia chama cha muungano wa Azimio la Umoja dhidi ya mpinzani wake Willium Ruto na Kushindwa.
Baada ya kutangazwa matokeo hayo kutolewa Agosti 15, na kumtangaza Willium Ruto wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) mshindi, Raila Odinga kupitia mkutano mfupi alitangaza kuwa matokeo ni batili na kupeleka shitaka hilo mahakama kuu ili lipitiwe upya.

Mapema tarehe 5 ya Mwezi Septemba, mahakama iliyokuwa inashughulika na shitaka hilo ilitoa maamuzi kuwa ushindi wa Ruto ulikuwa halali na matokeo hayakuwa batili na hivyo kumtangaza Willium Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya.
Kushindwa kwa Raila Odinga kwa mara ya tano kunamfanya atimize miaka 25 tangu aweke nia ya kugombea urais kwa mara ya kwanza mwaka 1997
Imeandaliwa na SIMON J. MOLANGA kwa msaada wa mtandao.