×

Viongozi wa Pakistani Wanajitahidi Kuzuia Ziwa Kubwa Zaidi Kufurika Kutokana na Mafuriko

Mafuriko Pakistani

katika mkoa wa kusini-mashariki wa Sindh viwango vya maji katika ziwa la Mancher vilionekana kupanda Zaidi na kuonekana kuwa vya hatari baada ya mvua kunyesha kwa muda mrefu ambazo ni mvua za masika ambazo zimepelekea takribani ya watu milioni moja kukimbia makazi yao.

 

Waziri wa umwagiliaji wa jimbo hilo aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kiwango cha maji katika ziwa hilo “hakijashuka” taarifa hizo alizitoa siku ya jumatatu.

 

Mkoa wa Sindh unazalisha nusu ya chakula nchini humo, na hivyo kuzidisha hofu kwamba wengi watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika nchi ambayo tayari inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi.

Mafuriko Pakistani

Mafuriko nchini Pakistan yameathiri takriban watu milioni 33 na kuua takriban 1,314, wakiwemo watoto 458, Shirika
la Kitaifa la Kudhibiti Majanga la Pakistan lilisema.

 

Imeandikwa:leocardia charles kwa msaada wa mitandao.

 

Imeandikwa: leocardia chaarles kwa msaada wa mitandao.

Leave a Comment