
Bei za Mafuta katika soko la dunia za Julai 2022 zimepungua ikilinganishwa na bei hizo kwa Juni 2022. Hivyo, bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua vilevile kwa kati ya shilingi 271/lita na shilingi 362/lita kwa petroli na kwa shilingi 430/lita kwa mafuta ya taa ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022.
Kwa mafuta ya dizeli, ukiiacha bei ya Tanga ambayo inashuka kwa shilingi 13/lita, bei za Septemba 2022 zimeongezeka kwa shilingi 37/lita na shilingi 86/lita kwa Dar es Salaam na Mtwara, sawia, ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Septemba 5, 2022 na Mkurungenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato bei za mafuta zinaonekana kushuka ukilinganisha na bei zilizokuwa zikitumika mwezi Agosti, Kushuka kwa bei hizi kunakuja baada ya bei hizo kupanda mfululizo kwa miezi mitano kuanzia Aprili mwaka huu.
