×

Umoja wa Mataifa UN Wasema Wanawake 131 Walibakwa Ndani ya Miezi Mitatu Sudan Kusini

Wanawake nchini Sudan Kusini

KATIKA ripoti iliyotolewa na Umoja wa mataifa UN pamoja na shirika la haki za binadamu imesema kuwa wanawake 131 walibakwa katika kipindi cha miezi mitatu.

 

Ripoti hiyo inaongeza kusema kwamba karibu raia 200 wameuwawa kwenye jimbo lililotatizika la Unity, katika muda wa miezi mitatu. Mashirika hayo mawili yameorodhesha ukiukwaji wa haki za kimataifa za binadamu pamoja na sheria za kimataifa za haki za binadamu kwenye jimbo la Unity nchini humo.

 

Ukatili huo unasemekana kutokea wakati wa mapigano kati ya vikosi vya serikali vikishirikiana na makundi rafiki yenye silaha, dhidi ya vile vya SPLM/IO ambavyo ni vitiifu kwa makamu wa rais Riek Machar.

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini

UNMISS ilisema Aprili kwamba takriban watu 72 waliuwawa Sudan kusini, huku wasichana 64 pamoja na wanawake wakibakwa kati ya Februari na Aprili kwenye kaunti ya Leer kwenye jimbo la Unity.

 

Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Leave a Comment