
KIM aliapa nchi hiyo haitaacha kamwe silaha zake za nyuklia na akasema hakuwezi kuwa na mazungumzo juu ya kutokomeza nyuklia huku akipongeza kupitishwa kwa sheria hiyo, vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimeripoti leo Ijumaa.
“Kutokana na sharia za nyuklia sisi tutatumia silaha hizo kama njia mojawapo ya ulinzi wwa taifa” alisema Kim

“maadamu silaha za nyuklia zipo duniani na zinatengenezwa hivyo basi tutaendelea kuongeza nguvu kwenye nyuklia japo marekani na wafuasi wake wanashinikiza sisi kuacha” aliongezea Kim Jong Un.
Wakati huo huo, Marekani imezidi kuwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inaweza kuwa inajiandaa kufanya jaribio lake la kwanza la nyuklia la chini ya ardhi katika miaka mingi iliyopita.
Imeandikwa:Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao