
MAFURIKO yaliyoikumba Pakistan tangu Juni, mwaka huu yameiletea nchi hiyo maafa makubwa kwa kuathiri mamia ya vijiji katika sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba ya nchi hiyo, maafisa wa Pakistan wameonya kuwa huenda ikachukua miezi mitatu hadi sita ya mvua kunyesha.
Katika Mkoa wa Sindh, upande wa kusini maji ya mafuriko yamebadilisha mashamba kuwa kama ziwa huku Maafisa wa Pakistan wakionya kuwa huenda ikachukua miezi mitatu hadi sita, ya mafuriko kupungua.

Hadi kufikia sasa, karibu watu 1,500 wamefariki ikikadiriwa kuwa nusu yao ni watoto na zaidi ya milioni 33 wamehamishwa katika makazi yao kutokana na mafuriko, ambayo yalisababishwa na mvua kubwa ya monsuni.
Maelfu ya watu wamepata hifadhi katika shule na majengo ya umma au kando ya barabara, tuta za mifereji kwenye mahema ya lami na kamba, ambapo wengi wa wale ambao vijiji vyao vina unafuu wamebaki majumbani mwao, wakiwa wamezuiliwa.

Mamlaka ya hali ya hewa ya nchi hiyo, imewataka watu kuondoka katika vijiji vilivyotengwa, na kuonya kwamba kusalia kwao kunaweza kulemea juhudi za misaada ambazo tayari zimedhoofika na kusababisha uhaba wa chakula pia kukithiri kwa maradhi ya malaria, homa ya dengue na magonjwa yatokanayo na maji.
Imeandikwa na: Oswald Mwesiga kwa msaada wa mitandao.