×

Zari Atajwa Kuwachukia Hamisa na Tanasha Kisa Kipo Hapa, Diamond Atajwa

Mwanamama tajiri Afrika Mashariki, raia wa Uganda mwenye maskani yake Durban nchini Afrika Kusini, Zari The Boss Lady.

Hamisa Mobeto; ni mwanamitindo wa kimataifa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye ameibua mjadala mzito akidaiwa kuibua tuhuma nzito dhidi ya baby mama mwenzake kwa msanii Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady.

 

Hamisa, Zari na Tanasha Donna; wote wamezaa na Diamond, lakini kumekuwa na madai kwamba, wawili kati yao wanaelewana, lakini mmoja anawachukia wenzake.

 

Inafahamika kwamba, pamoja na wote kuzaa na Diamond, lakini Hamisa na Tanasha ni marafiki ambao wamekuwa wakipeana kampani na kutamani kuwakutanisha watoto wao, Dyllan na Naseeb Junior, jambo ambalo Zari hataki kulisikia.

Hamisa Mobeto; ni mwanamitindo wa kimataifa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania.

Katika moja ya mahojiano yake, Hamisa anakaririwa akisema kuwa, yeye na Tanasha wapo sawana wanawasiliana vizuri na wapo tayari kukutanisha watoto wao, lakini tatizo lipo kwa mwenzao ‘mke mkubwa’, Zari.

 

“Mimi na Tanasha Donna tupo sawa na tunawasiliana sana, ila tatizo lipo kwa mwenzetu (Zari), labda hapendi kuwaweka watoto karibu, ila haina shida,” anasema Hamisa.

Mwimbaji na mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Tanasha Donna.

Chuki ya Zari dhidi ya Hamisa ilikuja baada ya kuchepuka na Diamond na kupata naye mtoto akijua fika kwamba jamaa huyo yupo naye kwenye uhusiano ulioshiba akiwa amembebea mimba ya mtoto wa pili.

Tangu hapo, Zari na timu yake hawakumuacha salama Hamisa kwani wamekuwa wakimshambulia asubuhi, mchana na usiku.

STORI NA SIFAEL PAUL

NDOA YA MANARA KUMEKUCHA, MGAWANYO MALI ZA HARMONIZE NA SARAH | HOTPOT

Leave a Comment