Kamwe: Nimeshuhudia Ukubwa wa Yanga Kwa Muda Ambao Nimefanya Kazi – Video
AFISA Habari wa Yanga, Ally Kamwe leo Oktoba 4, 2022 amesema marafiki wake wanamchukulia tofauti tangu alipojiunga na klabu hiyo akibainisha kuwa wamekuwa wakiishi naye tofauti na walivyokuwa wakiishi naye mwanzo.
Ally Kamwe amebainisha hayo kwa kudai kuwa hali hiyo imetokana na namna ya ukubwa wa taasisi anayoifanyia kazi kwa sasa.
Pia amesema kwa muda mfupi wa siku tatu ambazo amefanya kazi kama Afisa Habari ameshuhudia ukubwa halisi wa klabu hiyo kwani kuna mabadiliko makubwa yametokea katika Maisha yake na tasnia pia.