×

Mwenyekiti UVCCM Sengerema Kuja na Vipaumbele Vitano

Mwenyekiti wa Wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Sengerema Patric Mundeba amesema anakuja na vipaumbele vitano kuinua Jumuiya hiyo.
1. Nitasimamia kuundwa kwa vikundi vya vijana vyenye mlengo wakujiinua kiuchumi kila kata nakuhakikisha vinarasimishwa ili kunufaika na mikopo yenye riba nafuu haswa ile asilimia 4 inayotolewa katika kila halmashauri.
2. Nitafuatilia fursa zilizo rasmi na zisizokuwa rasmi zakiuchumi kuhakikisha vijana wa wilayaya Sengerema wananufaika navyo, mfano fursa ya ziwa victoria kwa vijana kujishughulisha na uvuvi, fursa za mgodi unaotarajiwa kufunguliwa hivi karibu wilaya hapa na fursa nyinginezo.
3. Tutawagusa pia vijana katika Michezo na sanaa ili kujenga urafiki na nahusiano mazuri ndani ya jamii.
4. Nitasimama hadharani  kupinga dhuruma, uonevu na uminywaji wa haki dhidi ya vijana bahati nzuri ninayo taaluma ya Sheria hilo halitonipa shida kwani chama chetu kinaamini katika usawa kwa binadamu wote na kuheshimu utu wa mtu.
5. Tutahakikisha elimu ya ujasiriamali inawafikia vijana kuwatengenezea utayari wakujitegemea.
Nafahamu changamoto kubwa ya vijana ni suala la uchumi wao kuimarika, hivyo nimejipanga vizuri katika kipindi changu kuhakikisha kiu yao inapata suluhu kama sio ahueni, kikubwa wanipe ushirikiano.

Leave a Comment