
Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imetangaza kupunguza gharama za tozo za miamala ikiwa ni kuitikia wito wa maelekezo ya yaliyotolewa hivi karibuni na serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango kwa watoa huduma kupunguza tozo za miamala ya simu ili kuwezesha wateja kufaidika na huduma hiyo kwa punguzo la hadi asilimia 50%.
Serekali ilitoa maelekezo kufanya marekebisho ya punguzo la Tozo ya serikali zinatozwa kwa wateja wa huduma za fedha kwa njia ya simu (Mobile Money) kwa lengo la kuendelea kurahisisha huduma hiyo ili kufikia malengo ya kukuza na kupanua huduma hiyo kila mahali.

Punguzo kubwa la tozo katika kutuma au kutoa fedha kupitia Airtel Money imeendelea kuongeza unafuu kwa watumiaji wa huduma ya Airtel money na Sasa Ni Kama zamani.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo hii kwenye makao makuu ya kampuni ya Ariel Tanzania Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda amesema huu ni mwendelezo wa kuwajali na kuwapunguzia gharama wateja wake.
Kwa Upande wake Meneja chapa wa Airtel money Bi Gillian Rugumamu ameelezea kuhusu Airtel ilivyojidhatiti katika kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na mteja kujihudumia yeye mwenyewe kama anavyofafanua
Nchunda aliongeza kuwa “Airtel Money tunasonga mbele na dhamira yetu ya kuwahudumia wateja wetu wote kwa gharama nafuu na kuwafikia pia wateja ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa kusogeza huduma za Airtel Money Branch kila kona ya Tanzania, sasa tunajivunia kuwa na zaidi ya Airtel Money Branch 3000 nchi nzima”.
Airtel Money imekuwa ni huduma ya fedha kwa njia ya mtandao inayojipambanua kwa upekee kwa kutanuka Zaidi kwa kuwa na wakala zaid ya 160,000 waliosambaa nchni kote wakihudmia wateja masaa 24 siku 7 za wiki kama njia mojawapo ya ajira.