
KUNA makampuni mengi ya teknolojia ya simu yanayofahamika duniani ikiwemo Google Pixel, Apple na Samsung, Kampuni hizi zipo katika mashindano kwenye soko la bidhaa za Simu ingawa kwenye akaunti ya Google Pixel ya twitter imeonekana kutumika kumjibu Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Apple.
Mtu aliyekuwa anaishikilia akaunti hiyo ya Google Pixel kwa wakati huo alijibu hiyo tweet kwa kutumia simu ya iphone kitu ambacho hakifai kwa sababu kuzingatia kuwa ni katumia simu ya kampuni ambayo wapo nao kwenye ushindani hivyo haileti picha nzuri kwa wateja hao ambao wanajaribu kuwavuta kwenye ulimwengu wa bidhaa za kampuni ya Google Pixel.
Hili tukio limekuwa ni kitu kinachoongelewa sana lakini sio jambo la kushangaza kwa kuwa hata mwaka 2018, kampuni ya simu ya Samsung ilimshtaki balozi wa chapa wa nchi ya Russia millioni $1.6, sababu alitumia iPhone X badala ya bidhaa yao aliyopewa kuitangaza na kampuni hiyo.

Hivyo kwa upande mwingine watu hawajashangazwa sana na tukio hilo, katika ujumbe huo ulioandikwa twitter ulimlenga Tim Cook huku akaunti hio ikitumia alama ya reli ya #TakeNote kudhihirisha ushirikiano wa kampuni hio ya Simu na wachezaji wa mpira wa kikapu NBA ambao wanahusika kwenye kuzitangaza Simu zao Google ziitwazo Google Pixel 7 na Google Pixel 7 Pro.
Baada ya tukio hili kutokea imedhihirisha kuwa karibia watu wote wanapendelea kutumia simu za iPhone ikiwemo hata wapinzani wao Google, haijafahamika Google itachukua hatua gani kwa mfanyakazi huyo, mwaka 2013, kuna wafanyakazi wa Huawei walioshushwa vyeo na kukatwa $728 kwenye mishahara yao kila mwezi kwa kufanya kosa la kutangaza kampuni hiyo kwa kutumia simu ya iPhone.
Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem Kwa msaada wa mitandao