The House of Favourite Newspapers

Masha Love, Jimmy Mafufu Wachafua Hali Ya Hewa Wadaiwa Kuwa Kwenye Uhusiano

0

Masha Love; ni video vixen na Jimmy Mafufu ni muigizaji maarufu nchini Tanzania; wawili hao wamechafua hali ya hewa.

Balaa zito wikiendi iliyopita lilikuwa ni suala la Masha Love kumuanika vibaya Jimmy Mafufu.

 

Kwa mujibu wa Masha Love, alikuwa mchepuko wa Jimmy Mafufu.

Wawili hao wanadaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa siri mno, lakini mimba ikatibua mambo.

Kwa mujibu wa Masha, mimba iliingia na hapo ndipo matatizo yakaanza kutokea kwani Masha Love alitaka kuzaa huku Jimmy Mafufu akiwa hataki.

 

Inadaiwa kwamba, Jimmy Mafufu ambaye pia ni mchungaji alitaka mimba itolewe maana yeye ana mke na watoto hivyo kuzaa nje ya ndoa kwa Mkristo ni kukiuka au kuvunja kiapo cha ndoa.

 

Inasemekana kuwa, kilichomkasirisha Masha Love ni suala la kutoa mimba, kwani yeye hayupo tayari ndiyo maana akaamua kumuanika Jimmy Mafufu kwenye mitandao ya kijamii.

 

Masha Love ameandika waraka huku akivujisha meseji, chatting, voice note na video za Jimmy ambazo anamtaka atoe mimba hiyo.

 

Mbali na hayo, Masha Love anadai kwamba Jimmy Mafufu amempiga na mara nyingi alikuwa akimuomba kumuingilia kinyume na hivi sasa amempiga block kila sehemu.

 

Masha Love anasema; “Wacha ifike muda niongee ukweli na dunia ijue nimekuvumilia sana na kukuheshimu ila sasa unaniona mimi mjinga, unanifanyia mambo ya kijinga ukiamini kuwa labda mimi ni taahira, chizi siwezi kufanya lolote.

 

“Najua wewe ni mtu mzima na una familia na unajiheshimu pia una mtoto wa kike, vaa viatu vyangu mtoto wako akifanyiwa mambo kama haya kwa hili sitakuacha, nitahakikisha naweka bayana yako yote hadharani.

 

“Ulikuja kwangu kwa maneno mazuri na mambo kibao kuniahidi malipo yake unanijibu jeuri na kuni-block ukidhani umewini, sasa nina video zako za ndani tukiwa wote ushahidi wa SMS na voice note zote, wacha dunia ijue wewe ni mnyama.

 

“Kiasi gani uliyejifunika katika kimvuli cha kujifanya unamjua Mungu. Jimmy Mafufu wewe ni nyoka mbwaa…mbwaa hufai kabisa sasa kama hii mimba ni yangu na mimi ndiyo nitajua namalizana nayo vipi na sitakusumbua, eti nitoe mimba, je, wewe mama yako angetoa mimba ungelala na mimi saa ngapi?

 

“Ila ninachotaka dunia ijue wewe baba ni malaya kiasi gani na ni katili mwenye roho mbaya ni mara kadhaa umekuwa ukinilazimisha kufanya kinyume na maumbile nimekukatalia ila fadhila zake eti unakataa mimba na kusema utanionyesha na nitakoma, sasa kipigo ulichonipa hakitoshi kukoma sasa nasema tutaonyeshana kama mbwai na iwe mbwai na nitatoa kila kitu huu ni mwanzo tu.”

 

Kwa wanaomjua Masha Love, ni miongoni mwa wanawake ambao huwa hawajali watu watamsema nini hivyo hufanya mambo ambayo husababisha azungumziwe kama ishu ya kutikisa manyonyo.

 

Watu wanahoji, hivi mtu unajua kabisa unayechepuka naye ana mke na watoto halafu unajipatisha mimba yake?

Hata hivyo, watu wanaoijua ishu hiyo vizuri wanasema kuwa, Masha amemdhalilisha Jimmy kwani anajulikana ni Mtumishi wa Mungu.

Leave A Reply