
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameguswa na suala la maji kukosekana sehemu mbalimbali na hata kutoa ufafanuzi.
Ametoa sababu yakuwa shughuli za kibinadamu ndio chanzo kikubwa kwani kuna watu wanalima, wanakata miti, na wengine wanafuga samaki na kupitia hayo yote maji yanapungua.
Aidha amewata viongozi husika kushughulikia suala hilo kwa undani zaidi ili kuleta ahueni katika jamii.
Rais samia ameyasema hayo leo Novemba 1, 2022 alipokuwa akishiriki katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la Nishati safi ya kupikia.