×

Kongamano Kubwa la Vijana Kufanyika UDSM, Novemba 12, 2022

 

Zaidi ya vijana 500, kesho Jumamosi wanatarajia kushiriki kwenye Semina ya siku moja iliyoandaliwa na FD360 ya tukio la fursa kwa vijana kukutana na watu wanao watizama kama mfano ambalo litafanyika bila kiingilio kwenye ukumbi wa New Library unaopatikana ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).



Semina hii itahusisha watu mbalimbali Akiwemo Mkurugenzi wa Masoko wa Metl Fatema Dewji, mwimbaji wa Bongo Fleva Jux, mwigizaji Idris Sultan Pamoja na Wafanyabiashara Anthony Luvanda na Given Edward.



Semina hiyo inalenga kujifunza kutoka kwao kuhusu namna ya kutengeneza chapa binafsi na kupata wasaa wakufahamiana nao kwa undani Zaidi.

Leave a Comment