×

Aguero: Arsenal Wana Kikosi cha kuwashinda Man City na Kushinda Ubingwa wa Premier

Staa wa zamani wa Manchester City, Sergio Aguero.

 

STAA wa zamani wa Manchester City, Sergio Aguero amesisitiza kuwa anaamini Arsenal ya msimu huu ina kikosi imara cha kuweza kuwashinda Man City na kushinda ubingwa wa Premier.

 

Aguero amepinga imani ya wengi kwamba Arsenal hawana uwezo wa kushinda ubingwa wa Premier kutokana na ubora wa kikosi cha Man City, licha ya kushinda michezo yao 11 kati ya 13 msimu huu wakiizidi Man City kwa pointi mbili na pointi 11 mbele ya Manchester United walio kwenye nafasi ya pili.

 

Licha ya fomu hiyo wengi wanaamini huenda Arsenal wakapata majeraha na kutetereka kwa kukosa kikosi kipana. lakini Aguero aliyeshinda mataji matano ya Premier akiwa na City anaamini Arsenal bado wana kikosi imara.

Wachezaji wa timu ya Arsenal.

 

Kuhusiana na hilo Aguero alinukuliwa akisema: “Arsenal wamekuwa kwenye kiwango bora sana msimu huu na kuonyesha upinzani mkubwa dhidi ya City. wana kikosi bora cha kuweza kushinda ubingwa, lakini Liverpool licha ya magumu yao wanaonekana hawako mbali ni suala la kusubiri kuona nini kitatokea baada ya Kombe la Dunia.

 

“Kuna dirisha la usajili la mwezi Januari na kama Arteta ataona anahitaji maboresho anaweza kufanya usajili, lakini sidhani kama wana kikosi kidogo, kwani hivi karibuni aliumia Bukayo Saka na hawakutetereka.”

 

VILIO: MWILI wa MREMBO MTANZANIA ALIYEFARIKI INDIA WAZIKWA KIJIJINI KWAO IRINGA…

Leave a Comment