×

Kampuni ya  GF Yajivunia Mafanikio ya Miaka 15, Kuwa ya kwanza Kuteneneza Magari Nchini

Naibu Waziri wa , Uchukuzi na mawasiuliano , Atupele Mwakibete  akimkabidhi cheti cha udhamini mkuu,Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd, Ally Jawad Karmal  wakati wa uzinduzi wa Chama cha  wamiliki wa matipa na mitambo (TTMA) uliofanyika jijini Dar es Salaam .

 

Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd  inajivunia mafanikio iliyoyapata kwa kipindi  cha miaka 15  katika sekta ya uuzaji  wa magari ya Mizigo na Mitambo nchin.
 Hayo yamesemwa  wakati wa uzinduzi wa chama cha wamiliki wa Magari ya mizigo na mitambo nchini katika hafla iliyofanyika jijini Dar es saaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa kitengo cha Biashara na masoko wa kampuni ya  Gf Trucks & Equipment’s Ltd ,Salman Karmal alisema kutokana na sheria za uwekezaji nchini kuwa rafiki wao kwa kipindi cha miaka 15 wameweza kufungua kiwanda cha  kuunganisha magari , GF Vehicle Assemblers  kilichpo Kibaha mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na mawasiliano, Atupele Mwakibete  akizungusha kifaa maalumu kuashiria uzinduzi wa  Chama cha wamiliki wa matipa na mitambo (TTMA) jijini Dar es salam .Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd, Ally Jawad Karmal  kushoto ni Salman Karmal mkuu wa kitengo cha Biashara na masoko wa GF   na Kulia ni Mwenyekiti wa Chama (TTMA) Emmanuel Moshi

 

Pia lisema wa kwa kuunda chombo cha pamoja  ni hatua moja wapo katika sekta ya usafirishaji kwani kupitia umoja huo tyr itakuwa rahisi chamngamoto zao kutatuliwa kwani hapo awali walikua hawana jukwaa la pamoja na kuwasemea tofauti na tasnia zingine   na wao GF kama walezi wa umoja huo watakua bega kwa beka kuhakikisha unakuwa na tija kwa taifa kwa ujumla.

 

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Matipa Tanzania (TTMOA), Emmanuel Moshi aliiiomba Serikali ili kuwanufaisha wakandarasi wazawa kwenye miradi inayoendelea nchini, kabla ya mipango ya utekelezaji waitwe watoe maoni yao.
Alisema kupitia TTMOA wanauwezo wa kutekeleza miradi mikubwa ya Serikali na hakuna haja kuyatumia makampuni ya nje kutekeleza miradi hiyo.
“Tunaiomba Serikali iangalie umuhimu wa mitambo hii inayoingizwa nchini,tunalipa kiwango kikubwa cha kodi,”alisema. Chama Cha Wamiliki wa Mitambo Tanzania kilianzishwa mwaka 2018  na mpaka sasa kina wanachama 150.
Wadhamini waku wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa
Kwa upande wa serikali  Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Atupele Mwakibete aliwata wakandarasi wote nchini kuhakikisha wanaimarisha Umoja wao kupitia chama hicho.
“Ili mambo yaende vizuri ni lazima muwe katika Umoja, kupitia chama hiki Serikali itaendelea kuwasiliza, wakandarasi wote wenye magari, wasio na mitambo hata wale wasio wakandarasi na wanamiliki mitambo wajiunge na chama hiki penye umoja kuna maendeleo,”alisema.
Mwakibete alisema ili taifa liendelee linahitaji ujenzi hivyo TTMOA ni nguzo muhimu kwani imechagua upande ambao Serikali inaweka nguvu.

Leave a Comment