×

Maandamano Makubwa Yazuka China, 10 Wafa kwa moto, Wataka Rais Xi Jinping Ajiuzulu

Maandamano dhidi ya masharti Covid nchini China yanaonekana kushamiri kufuati moto ulioua watu 10 katika jengo la ghorofa huko Urumqi.

Katika jiji la Shanghai, video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na waandishi wa habari wa kigeni zinaonyesha maelfu ya watu wakiingia barabarani kuwakumbuka walioathiriwa lakini pia kuandamana dhidi ya vizuizi vya Covid.

Mamia walisikika wakimtaka rais Xi Jinping ajiuzulu.

Watu wengi wamelaumu vifo vimesababishwa na kufungwa kwa majengo hayo ya makazi.

Mamlaka ya Uchina imekanusha kuwa ndio sababu. Ingawa mamlaka ya Urumqi iliomba msamaha usio wa kawaida mwishoni mwa Ijumaa – wakiapa kumwadhibu mtu yeyote ambaye hajatekeleza wajibu wake.

Katika mkusanyiko huo mjini Shanghai, wengine walisikika wakipiga kelele kama vile “Xi Jinping, ng’atuka” na “Chama cha Kikomunisti, ng’atuka”.

MBOSSO AKATIKA MAUNO HADI CHINI, CHEKI WAREMBO WALIVYOSHINDANA NAYE STEJINI, KIDIMBWI PARTY…

Leave a Comment