Mwigizaji wa tamthilia ya Squid Game, O Yeong-su mwenye umri wa miaka 78, amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono, ambapo anatuhumiwa kumgusa isivyofaa mwanamke mmoja mwaka 2017.
Kufuatia shtaka hilo, Wizara ya Utamaduni ya Seoul imeripotiwa kuacha kurusha matangazo ya serikali yanayomuhusisha mwigizaji huyo.
Hata hivyo Bw. O Yeong-su amekanusha mashtaka hayo.