×

Mawakala wa Bima Wafanya Mkutano Kujadili Changamoto, Kamishna Awaahidi Neema

Mkutano ukiendelea.

 

Dar es Salaam 7 Desemba 2022: Viongozi wa mawakala wa bima nchini kutoka kanda tano za Tanzania Bara pamoja na Zanzibar leo wamefanya mkutano mkuu kujadili changamoto ya kazi zao.

Kamishna Mkuu wa Bima nchini, Baghayo Saqware akizungumza kwenye mkutano huo.

 

Mawakala hao pamoja na kujadili changamoto hizo waliziwakilishwa kwa Kamishna Mkuu wa Bima nchini, Baghayo Saqware aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano.

Mmoja wa viongozi wa mawakala wa Bima nchini, Chuki Shabani akimuelezea mgeni rasmi (hayupo pichani) changamoto zinazoikabili tasnia yao.

 

Akizungumza na viongozi hao wa mawakala kamishna Saqware alianza na kuwapongeza mawakala hao kwa kuendelea kutoa huduma za kiuminifu kwa wateja wao na kuwaambia kuwa changamoto zao zote amezipokea na kuwaahidi kuzifikisha kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa waziri kwa ajili ya kuzifanyia utatuzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Bima nchini, Sayi Daudi akibadilishana mkataba na Wakala wa Bumaco, Bw. Mzava ambao ndiyo watakaotoa huduma ya bima kwa mawakala. Anayeshuhudia katikati ni Kamishna wa Bima nchini, Baghayo Saqware.

 

Viongozi hao wa mawakala hao kwa kuonesha kujali umuhimu wa bima nao wamezindua mfuko wao wa bima itakayotolewa na Bumaco kwa ajili ya familia zao na watumishi wao.

 

Kamishna huyo aliwataka viongozi hao kuboresha mazingira ya ofisi kwani neema zaidi inakuja ikiwemo kuanza kutoa huduma ya bima ya afya ambayo inatarajiwa kuwa kwa kila mwananchi. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL

Leave a Comment