×

Timu ya Taifa ya France Yawasili jijini Paris Ikitokea Qatar Yapokelewa Kishujaa

Timu ya taifa ya France imewasili salama jijini Paris ikitokea Qatar na kupokelewa kishujaa na wafanyakazi wa uwanja wa Ndege pamoja na Mashabiki.

Kocha Didier Deschamps na nahodha Hugo Lloris ndio walikuwa wakwanza kushuka kutoka kwenye ndege hiyo ya shirika la ndege la Air France iliyokuwa imezungukwa na waandishi wa habari wakiwemo wapiga picha.

Akizungumzia mustakabali wa uongozi wake Deschamps amesema “nina huzuni sana kwa ajili ya wachezaji na wafanyakazi. Nitakuwa na mkutano na Rais wa Shirikisho la soka mwanzoni mwa mwaka ujao, baada ya hapo mtajua kitakachofuatia.”

Kikosi hicho kilichukuliwa na basi maalumu na kupelekwa mjini ambako kilipokelewa rasmi nyumbani na mashabiki.

KAMATI YA MAADILI YA TFF YAFANYA MAAMUZI SHAFFIH DAUDA KUENDELEA KUTUMIKIA ADHABU YAKE

Leave a Comment