Rais Samia Awapisha Viongozi Wateule Ikulu Chamwino
January 9, 2023 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Januari 09 2023
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Januari 9, 2023 amewapisha viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
Waliapishwa ni pamoja na Dkt. Natu El-Maamry Mwamba Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Ndugu Griffin Venance Mwakapeje ameapishwa kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Emmanuel Mpawe ameepishwa kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.