×

Mamia ya Watu Wafariki Dunia Kwa Tetemeko Kubwa Uturuki na Syria

 

Zaidi ya watu 100 wamefariki dunia nchini Uturuki na wengine 230 nchini Syria kufuatia tetemeko kubwa lilizoipiga nchi hizo, likiwa na ukubwa wa magnitude 7.8.

 

Tetemeko hilo limetokea alfajiri ya leo, Jumatatu, Februari 6, 2023 ambapo mji wa viwanda wa Gaziantep nchini Uturuki unatajwa kupata madhara zaidi huku nchi nyingine jirani za Lebanon, Cyprus na Misri, zimekumbwa na tetemeko hilo ingawa zenyewe hazijapata madhara.

 

 

 

Inaelezwa kwamba tetemeko hilo limeanzia Kusini mwa Uturuki na kusambaa kwa kasi mpaka Kaskazini mwa Syria na kusababisha maafa makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka ya karibuni katika nchi hizo mbili.

 

Ahmed Damiriyye, msaidizi wa Wizara ya Afya nchini Syria amesema mpaka sasa waliopoteza maisha nchini humo ni 237 huku wengine 639 wakijeruhiwa na kueleza kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na watu wengi kufukiwa na vifusi vya majengo yaliyobomolewa na tetemeko hilo.

 

 

Vikosi vya uokoaji kutoka katika nchi zote mbili, vinaendelea kuwaokoa watu walionasa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka kutokana na mtikisiko uliosababishwa na tetemeko hilo.

 

Rais wa Syria, Recep Tayyip Erdogan, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter ametoa pole kwa wote waliopata madhara kutokana na tetemeko hilo.

Leave a Comment