×

Mwanadada Tems Ang’ara Tuzo za Grammy, Burna Boy Aambulia Patupu

 

Msanii mrembo kutoka nchini Nigeria, Temilade Openiyi almaarufu Tems, usiku wa kuamkia leo ameshinda tuzo ya Grammy katika kipengele cha Best Melodic Rap Performance ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza kupata tuzo hiyo tangu alipoanza muziki.

Tems ambaye alikuwa nominated kwenye tuzo tatu, ameibuka kidedea katika kipengele hicho, ikielezwa kwamba kilichompaisha ni ngoma ya Wait For U aliyoshirikishwa na Future pamoja na Drake ambapo uandishi wa mashairi yake na sauti yake, vimemfanya ang’are.

Wakati Tems aking’ara, Burna Boy kwa upande wake mambo hayajamwendea vizuri baada ya kushindwa kuondoka na tuzo yoyote, licha ya kuwa nominated kwenye categories 2 tofauti.

Leave a Comment