×

TBA Yadaiwa Kubadili Bei Za Nyumba Magomeni Kota, Wakazi 644 Wagomea Mkataba Mpya

Wakazi 644 wanaoishi Magomeni Kota wamegoma kusaini Mkataba wa Manunuzi ya Nyumba hizo kwa madai bei mpya walizopewa ni kubwa na haziendani na hali ya Uchumi wao

Wakazi hao wamesema bei mpya iliyowasilishwa ni kati ya Tsh. Milioni 48 kwa Chumba na Sebule hadi Tsh. Milioni 56 kwa Vyumba 2 na Sebule kwa malipo ya Miaka 15, kiwango ambacho wamedai ni kikubwa na ni mtego wa kuwafukuza

Kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Majengo (TBA), Bei iliyopendekezwa na Serikali Juni mwaka 2022 ya Tsh. Milioni 12 hadi Tsh. Milioni 17 kwa Malipo ya marejesho ya Miaka 10, haikukidhi thamani ya eneo, haikujumuisha Faida na Huduma za muhimu.

MAMIA WAFARIKI kwa TETEMEKO UTURUKI na SYRIA, VIFO VINAONGEZEKA, WENGI WAMEFUKIWA na VIFUSI…

Leave a Comment