Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (kulia), Mbwana Samatta (kushoto) sambamba na viongozi mbalimbali wa serikali na wadau soka wakiingia kwenye ukumbi wa Hyatt jijini Dar jana usiku kwenye hafla ya kumpongeza Samatta.
Kutoka kulia ni Waziri Lukuvi, Mbwana Samatta na Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.
Samatta katika picha ya pamoja na Wazriri Nape, Waziri Lukuvi na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia).
IKIWA ni kuthamini tuzo aliyotwaa nahodha wa timu taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ya Mchezaji Bora wa Soka Afrika kwa wachezaji wa ndani, Serikali kupitia wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, jana imemzawadia nyota huyo kiwanja cha kujenga makazi kilichopo eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujali na kuthamini heshima ambayo Samatta ameiletea Tanzania ya kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani (ligi za Afrika).
Samatta amepewa kiwanja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi kwenye sherehe maalum ya kumpongeza Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo hiyo iliyoipa heshima kubwa Tanzania, jana usiku Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mbwana Samatta aliishukuru serikali kwa kutambua mchango wake katika soka la ndani, sapoti ya serikali katika masuala ya soka na michezo kwa ujumla huku akiiomba serikali kuweka mikakati endelevu ya kuendeleza soka nakuibua vipaji zaidi ili wapatikane akina Samatta wengi zaidi.
Kwa upande mwingine, Samatta aliwashukuru Watanzania na wadau wote wa michezo wanaomuunga mkono. Samatta amesema amekuwa akifarijika tokea arejee nyumbani na tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika anayecheza Afrika kutokana na Watanzania kuendelea kumfariji.
…Lukuvi (kushoto) na Samatta wakiteta jambo.
…Hafla hiyo ikiendelea
Hafla na mazungumzo yakichukua nafasi
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akizungumza
Samatta akitoa neno la shukrani kwa Serikali na Watanzania wote kwa kumsapoti.
Waziri wa Vijana, Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye akimpongeza Samatta kwa mara nyingine.
Mgeni rasmi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimpongeza Samatta.
Mgeni rasmi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa niaba ya Waziri Mkuu, kassim Majaliwa akikabdhi zawadi kwa Samatta.
Samatta akikabidhi jezi yake kwa Waziri Lukuvi
Samatta akikabidhi jezi yake kwa Waziri Nape
Picha za pamoja na viongozi wa serikali na wadau wa soka

…Katika pozi na mwandishi wa Global, Musa Mateja
Thomas Ulimwengu akisalimiana na baba wa Mbwana Samatta, mzee Samatta
…Picha ya pamoja na wadau.
Kutoka kushoto ni Mshindi wa Big Brother Africa (BBA) 2014/2015, Idris Sultan, Mbwana Samatta na mdau wa soka.
…Samatta na mdau
Samatta akiweka pozi na Thomas Ulimwengu.