×

Rais Buhari wa Nigeria Aongeza Muda wa Kubadilisha noti ya 200 ya Naira kwa siku 60

Rais wa Nigeria Buhari ameiagiza Benki Kuu kuachilia noti za kale za 200 za naira tena katika ili kutumiwa sambamba na mpya hadi Aprili 10. Baada ya hapo noti hizo za zamani za naira 200 zitakoma kutumiwa.

Wakati huo huo, noti za zamani za naira 500 na 1000 si halali tena na lazima zirejeshwe Benki Kuu kupitia njia zilizoainishwa.

Taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika limeshuhudia maandamano yenye hasira katika miji huku watu wakihangaika kupata noti mpya.

Baadhi ya wateja katika eneo la Warri kusini mwa Nigeria na Benin City waliripotiwa kuchoma moto benki mbili za kibiashara.

Raia wa Nigeria wamekabiliwa na foleni ndefu kwenye mashine za kutoa pesa huku baadhi yao wakilala nje ya benki ili kujaribu kuwa wa kwanza kupata pesa.

YANGA YAIWEKEA MTEGO TP MAZEMBE, KWA MZUKA WA SIMBA MWARABU ANAKUFA 4 | KROSI DONGO

Leave a Comment