
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imetoa ufafanuzi wa taarifa iliyochapishwa na gazeti moja la kila siku likiwa na kichwa cha habari: ‘Madudu Tena Kitabu Kipya cha Hisabati’.
Taarifa iliyotolewa na Dk. Aneth Komba, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu, inaeleza kwamba kichwa cha habari hiyo ni cha upotoshaji kwa kuwa maneno yaliyotajwa hayaathiri ujifunzaji na ufundishaji.
Taarifa imezidi kuongeza kuwa maneno hayo pia hayapotoshi wanafunzi kama taarifa ilivyojieleza na kueleza kuwa sura ya kitabu inayolalamikiwa, imeandaliwa na kukidhi mahitaji ya muhtasari.
