×

SBL Yakabidhi Pikipiki Na Zawadi Kadhaa Kwa Washindi Wa Kampeni ya Pilsner Mikoa Mitatu

Meneja Maskoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti(SBL) kanda ya Ziwa Lonald Lyatuu(kushoto) akimkabidhi zawadi ya Simu janja mkazi wa Muleba mkoani Kagera Heinsten Tumaini baada ya kushinda promosheni ya Pilsner Lager Kapu la Wana kwangua ushinde, wakati wa hafla iliyofanyika mkoani Simiyu, katikati ni Meneja Mauzo wa SBL mkoani Simiyu Bruno Nkwabi.

Dar es Salaam, Jumamosi Machi 04th, 2023: Serengeti Breweries Limited (SBL) kupitia kampeniya  bia yake ya Pilsner lager iliyopewa jina la ‘ Kapu la wana’ imekabdihi zawadi ya pikipiki na zawadi nyingine kwa washindi saba katika droo yake ya pili ya kampeni hiyo iliofanyika mapema wiki iliyopita na kubaini washindi kutoka Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.

Kutoka  droo ya pili ya kampeni, washindi watatu waliondoka na simu za mkononi, washindi wengine watatu walipata seti za televisheni na mshindi mmoja  alizawadiwa pikipiki. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwa wakati mmoja katika kanda ya Ziwa, Kaskazini na Kusini ambako kampeni ya ‘Kapu la Wana’ inahusika.

Akizungumza katika hafla ya ukabidhiji mkoani Kilimanjaro, mshindi wa pikipiki hiyo, Lazaro Kileo alisema anafuraha kuibuka mshindi wa pikipiki hiyo kutokana na kampeni hiyo na kuongeza kuwa kampeni hiyo imekuwa msaada kwani inasaidia kuinua uchumi wa watumiaji wanapokuwa wakitunukiwa zawadi kama vile pikipiki ambazo wanaweza kuzitumia kujiongezea kipato, “kampeni hii imeonekana kuwa ya thamani kwetu watumiaji kwa sababu tunazawadiwa zawadi ambazo kwa namna moja au nyingine zinaendeleza maisha yetu na hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani Pilsner Lager inatujali watumiaji.”

Washindi wengine 3 wa kampeni ya ‘Kapu la Wana’ walioondoka na simu za kisasa ni Lucy Faustine (Korogwe), HeinstenTumaini(Kagera) na George Gerald (Katavi), huku wengine 3 waliopokea runinga za kisasa ni Abdul Msafiri (Arusha), Salumu. Nyanga (Simiyu) na Happy Venance (Iringa).

Akizungumza katika moja ya hafla za makabidhiano ya zawadi mkoani Kilimanjaro, Meneja Mauzo wa SBL mkoa wa Kilimanjaro, Abel Mushi aliwapongeza washindi hao akisema dhumuni la kampeni ya ‘Kapu la Wana’ ni kuwajengea uwezo watumiaji wanaofanya kazi kwa bidii kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali pindi watakaposhiriki katika kampeni hiyo,” alisema.

“Tunawathamini wateja wetu na, hii ndiyo njia yetu ya kuwatunza kwa kupenda na kuunga mkono chapa yetu, hii ni mara ya pili tunaendesha kampeni hii na kupitia kampeni hii tunataka kuwapa wateja wetu fursa ya kuinua maisha yao kwa njia moja au nyingine. kwa mfano mshindi wa pikipiki anaweza kuamua kuitumia ili kusaidia kuongeza mapato yake na kwa upande mwingine, washindi wa runinga mahiri na simu mahiri zawadi zao zitaendeleza ustawi wao wa kijamii.” 

Alitoa wito kwa watumiaji katika kanda za Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki katika kampeni na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo ya muda wa wiki 8 ambayo ilizinduliwa tarehe 2 Februari. Zawadi hizo ni pamoja na runinga mahiri, simu mahiri, pikipiki na zawadi kubwa ya gari ambalo ni jipya kabisa.

Akielezea jinsi ya kushiriki Mushi alisema, “baada ya kununua bia ya Pilsner, kwaruza ili kupata kadi ya zawadi. Ikiwa zawadi ni nambari ya msimbo itume kwenye namba 15320 k.m. andika kapu 4321 Iringa. (Ruka nafasi kati ya maneno) kisha SMS itatumwa kuthibitisha ushiriki na kupata nafasi ya kushinda.”

SBL imewekeza jumla ya Tzsh 36 milioni katika kampeni ya kuwapata washindi 22 hadi mwisho wa kampeni.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Rispa Hatibu

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya SBL

Simu: 0685 260 901

Barua pepe: [email protected]

Leave a Comment