
Watu saba wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria la Kampuni ya Sheraton lenye namba za usajili T 922 ADC iliyotokea katika Kijiji cha Mwilima Kata ya Kasamwa Halmashauri ya Mji Geita.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza namna ilivyotokea…
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela ametembelea majeruhi na kutoa pole ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali.
Kamanda amesema ajali hiyo ilitokea Machi 7, 2023 muda wa saa 10:30 jioni na kueleza chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi hilo.
Kamanda Berthaneema Mlay amesema basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mwanza kuelekea Ushirombo mkoani Geita ambapo dereva alipoteza ustahimilivu baada ya tairi la mbele kupasuka na basi kutumbukia darajani.
Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita ambapo majeruhi walipelekwa katika kituo cha Afya cha Kasamwa kwa huduma ya kwanza na baadaye kuhamishiwa Katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu zaidi…