×

Rais Samia Amhamishia Polepole Cuba Kuwa Balozi, Bakari Apelekwa Uturuki…

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya vituo kwa mabalozi wawili na kumteua balozi mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole amehamishwa kituo na kupelekwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Pia Rais Samia amemteua Luteni Jenerali Mstaafu, Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE).

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mohamed alikuwa balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Pia Rais Samia amemteua Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Leave a Comment