×

Watu Kadhaa Wahofiwa Kufariki Baada ya Basi la Burudani Kuacha Njia na Kugonga Daladala

Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Burudani lililokuwa likitokea mkoani Tanga, kugongana na daladala, tukio lililotokea Mbezi Luguluni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda, basi hilo inadaiwa lilikuwa katika mwendo wa kasi ambapo lilimshinda dereva na kupoteza uelekeo na kuhamia upande wa pili wa barabara na kuigonga daladala pamoja na bodaboda wakati likijaribu kulikwepa gari dogo lililokuwa linaingia barabarani.

Taarifa zaidi zitakujia.

Leave a Comment