
Serikali imekubali kuruhusu magari yanayofanya safari zake kupitia Wilaya ya Sikonge kutoka Jijini Dar es Salaama kuanza safari zake kati ya saa 9 na 10 usiku ikiwa watapenda.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Alhamisi April 13,2023 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalumu Taska Mbogo (CCM).
Hata hivyo Waziri amesema kinachowapasa wenye mabasi ni kupeleka maombi ya muda gani wanataka kuanza safari zao ili wakapite Sikonge muda ambao utaruhusiwa badala ya kulala.