×

Simba Waitambia Yanga Kwa Mkapa… Robertinho Aibuka Mbabe – Video

SISI siyo levo zenu! Hiyo ndiyo kauli pekee ambayo walikuwa wanaitoa mashabiki wa Simba baada ya kikosi chao jana Jumapili kupata ushindi kwenye mchezo wa dabi mbele ya Yanga.

Simba walipata ushindi huo wa mabao 2-0 ikiwa ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao kwa asilimia kubwa hawakuwa wanapewa nafasi ya kupata ushindi kutokana na uimara wa wapinzani wao.

Kikosi hicho cha kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kilipata ushindi huo ambao ni muhimu kwao kwa ndiyo wa kwanza wanashinda kwenye dabui tangu msimu wa 2019/2020.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na beki Hennock Inonga ambaye alifunga bao dakika ya kwanza ya mchezo akitumia krosi ya Shomari Kapombe ambaye alianzishiwa kona fupi. Bao la pili la Simba lilifungwa na Kibu Dennis dakika 32 ya mchezo huo kwa shuti kali akiwa ndani kidogo ya eneo la ulinzi la Yanga ikiwa ni baada ya kumzidi ujanja beki Bakari Mwamnyeto wa Yanga.

Gumzo la mchezo huo ni kipa wa Simba, Ally Salim ambaye licha ya kuwa ndiyo mchezo wake wa kwanza wa dabi hiyo lakini alionyesha uwezo wa juu wa kuzuia mashambulizi ya washambuliaji wa Yanga wakiwemo Fiston Mayele, Kennedy Musonda, Stephane Aziz Kin a Bernard Morrison.

Ushindi huo unamfanya kwa mara nyingine kocha Robertinho kuibuka mbabe dhidi ya kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye awali waliwahi kukutana kwenye mchezo wa Wiki ya Mwananchi na Robertinho akiwa na Vipers ya Uganda aliwafunga Yanga kwa bao 1-0.

Leave a Comment